Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Antonio José González Zumárraga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Antonio José González Zumárraga (18 Machi192513 Oktoba2008) alikuwaKardinali waKanisa Katoliki kutokaEcuador.

González Zumárraga alizaliwa Pujilí, Ecuador. Alipadrishwa kuwa kasisi mnamo Julai 29, 1951, baada ya kusomea katika seminari ya San José mjini Quito na Chuo Kikuu cha Kipapa cha Salamanca, Hispania, ambako alipata shahada ya uzamivu katika sheria za kanisa.

Aliwekwa kuwa Askofu Msaidizi waQuito mnamo Mei 17, 1969 (akiwa na jimbo la kihistoria la Tagarata) na alitawazwa kuwa askofu mjini Quito mnamo Juni 15, 1969, na Kardinali Pablo Muñoz Vega, SJ, Askofu Mkuu wa Quito.

Mnamo Juni 30, 1978, aliteuliwa kuwa Askofu wa Machala, na kisha kuwaAskofu Mkuu Msaidizi wa Quito mnamo Juni 28, 1980. Aliingia rasmi kushika hatamu kamili za Jimbo Kuu la Quito mnamo Juni 1, 1985.

Aliteuliwa kuwa Kardinali naPapa Yohane Paulo II mnamo 2001, akiwa Kardinali Kuhani wa Santa Maria in Via.

Makala hii bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuiongezea habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Antonio_José_González_Zumárraga&oldid=1390351"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp