Wakati wa kukutana na Wareno Ufalme wa Kongo labda ulikuwa na eneo lakm² 300,000 ukaunganisha robo ya magharibi ya Kongo (Kinshasa) pamoja na sehemu za Angola na Kongo (Brazzaville).
Manikongo mbalimbali walijenga uhusiano naUreno na Kongo ilikuwataifa la kushikamana na Ureno hadi kuharibika kwa uhusiano huo. Katika kipindi kiletaarifa mbalimbali ziliandikwa zinazotupa leo picha nzuri ya ufalme huo.
Baada ya wafalme kuwaWakristoWakatoliki na kujengwa kwakanisa kuu, jina la "São Salvador do Congo" (kwaKireno: "Mwokozi Mtakatifu wa Kongo") lilikuwa kawaida kwa mji mkuu wamilki.
Dola lingine la kusini lilikuwa lile la Ndongo, lililopambana na Wareno miaka 30 chini yamalkiaNjinga katikakarne ya 17.
Vita vya uhuru
Mwaka1966Jonas Savimbi alianzisha tapo laUNITA (kwaKireno:União Nacional para a Independência Total de Angola) kama harakati ya kukomboa Angola kutokaukoloni waUreno. UNITA ilikuwa moja kati ya harakati tatu zilizoshindana.
UNITA ilianza kama kikundi chakikomunisti kufuatana naitikadi yaMao Zedong. Uadui kati ya Wakomunisti waUchina naUrusi ulionekana katika mashindano ya UNITA dhidi yaMPLA (kwa Kireno: Movimento Popular de Libertação de Angola - Partido do Trabalho) iliyosaidiwa na Urusi.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe
Baada yauhuru mwaka1975 MPLA ilitawalamji mkuu na kuundaserikali rasmi lakini Savimbi aliendelea kuipinga.
Tarehe22 Machi2002, Jonas Savimbi aliuawa vitani. Muda mfupi baadaye UNITA na MPLA zilikubaliana kusimamisha mapigano. UNITA ilichukua nafasi ya chama cha upinzani. Hata hivyo taratibu za kidemokrasia zilichelewa hadichaguzi za miaka2008 na2012 na toleo la katiba mpya la mwaka2010.
Makala hii kuhusu maeneo yaAfrika bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuAngola kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.