Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Anga-nje

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muunganisho kati ya uso wa Dunia na Anga-nje. Mstari wa Kármán katika urefu wa kilomita 100 (62 mi) umeonyeshwa. Tabaka za anga huvutwa kwa kiwango, wakati vitu ndani yao, kama Kituo cha Anga cha Kimataifa, sio.

Anga-nje(kwaKiingereza outer space) ni eneo laulimwengu. Tofauti naanga yadunia yetu inayojazwa naangahewa ni yote nje yake. Sehemu kubwa za anga za nje ni nafasi ambayo inakaribia hali yaombwe. Katika tupu hii kunamagimba ya angani kamasayari,nyota,galaksi,nebula namawingu.

Wanasayansi hawaoni ya kwamba nafasi kati ya magimba ya angani ni hali yaombwe au tupu kabisa lakini kuna kiasi kidogo chautegili wahidrojeni pamoja namnururisho wasumakuumeme nanyutrino. Katikanadharia yafizikia kuna piamata nyeusi nanishati nyeusi ambazo hazikuthibitishwa bado.

Mipaka ya Anga-nje

[hariri |hariri chanzo]

Si rahisi kutaja kikamilifu mpaka baina ya angahewa na anga-nje la Dunia. Kuna majaribio mbalimbali kufafanulia mpaka huo. Wengine wanaona inaanza katika kanda latabakanje yaangahewa. Shirika laFederation Aeronautique Internationale linatajakimo chakilomita 100 naNASA inataja kimo chakilomita 80 ambazo ni takriban sawa na mpaka bainatabakakati natabakajoto. Hata hivyo,satelaiti zinazotumiaobiti za karibu hadi km 500 juu ya uso wa ardhi, bado zinaathiriwa na viwango vidogo vya hewa vinavyoenea hadi kimo kile.

Kwa upande mwingine mipaka ya nje ya anga haijulikani kabisa. Nadharia mbalimbali zinadai ama anga za nje halina mwisho, au kuwa anga za nje inaendelea kupanuka ilhali imefikia umbali wa takribanmiaka nurubilioni 13 -14.

Kufuatana na nadharia yamlipuko mkuu anga lilianza kama nukta likaendelea kupanuka hadi leo na kwa wakati ujao. Kufuatana na nadharia hii umbali kati dunia yetu na nyota inaendelea kuongezeka.

Upelelezi wa Anga-nje

[hariri |hariri chanzo]

Utafiti kamili wa anga-nje ni vigumu kutokana na ukubwa wake. Nadharia zote zinategemea vipimo vya nuru na mnururisho zinazofika duniani au karibu nayo. Njia nyingine ni kutuma vyombo vya angani kwenda safari ya anga za nje lakini kutokana na umbali mkubwa mno haziwezi kufika mbali kweli. Chombo cha angani kilishosafiri mbali hadi sasa niVoyager 1 iliyoondoka duniani mwaka 1977 na hadi sasa imepita sayari za Uranus na Neptuni. Chombo chaNew Horizon kiliondoka dunaini mwaka 2006 kiliipita Pluto mwaka 2015 na kuendelea hadi ndani yakanda la Kuiper.

Hali ya kisheria ya Anga-nje

[hariri |hariri chanzo]

Nchi zaUmoja wa Mataifa ziliundamkataba wa kimataifa juu ya anga za nje kwa azimio lamkutano mkuu wa UM mwaka 1963. 1967Umoja wa Kisovyeti,Marekani naUfalme wa Maungano (Uingereza) zilitia sahihi mkataba huu kama madola ya kwanza. Hadi 2008 nchi 98 zimeikubali kisheria na nchi 27 za ziada zimetia sahihi.

Katika mkataba huu zinapatana ya kwamba nchi zote zinaweza kupeleleza anga za nje lakini hakuna haki ya nchi yeyote juu yake. Inakataliwa upelekasilaha za nyuklia angani.

Mkata uliofuata wa 1979 juu ya mwezi unadai ya kwamba mamlaka juu ya magimba yote ya angani yawe mkononi wa jumuiya ya kimataifa. Lakini hadi sasa nchi zilizopeleka wanaanga nje ya angahewa hakuitilia sahihi.

Viungo vya Nje

[hariri |hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo yasayansi bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuAnga-nje kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Anga-nje&oldid=1302122"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp