Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Andy Warhol

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Andy Warhol mwaka 1977

Andy Warhol (jina la kuzaliwa niAndrew Warhola,6 Agosti1928-22 Februari1987) alikuwa kati ya wasanii mashuhuri waMarekani katika sehemu ya pili yakarne ya 20. Anakumbukwa kama mwanzilishaji wa mtindo waPop Art alioitekeleza katika picha na filamu.

Asili zake

[hariri |hariri chanzo]

AlizaliwaPittsburgh kwenye jimbo laPennsylvania. Wazazi walikuwa wahamiaji kutoka Slovakia baada yaVita Kuu ya Kwanza ya Dunia na baba alifanya kazi katika migodi yamakaa.

Msanii wa matangazo

[hariri |hariri chanzo]

Baada ya shule Andy alisoma uchoraji kwenye Carnegie Institute of Technology mjini Pittsburgh (sasa Carnegie Mellon University). 1949 alihamia New York City akawa mchoraji kwa ajili ya magazeti na biashara ya matangazo. Tangu 1952 alianza kuonyesha michoro yake katika maonyesho. Alipata jina nzuri akaajiriwa na kampuni ya muziki RCA Records na kutunga kawa kwasahani za santuri.

Kubuni Pop Art

[hariri |hariri chanzo]

Tangu 1960 alianza kutumia teknolojia ya kuchapisha kwa kutumia sten seli ya kitambaa.

Alitumia picha zilizopatikana katika mazingira ya kila siku. Aliona wasanii wenzake mara nyingi walichora picha zisizoeleweka na watu wa kawaida. Kinyume chake aliamua kutumia picha zilizopo katika mazingira ya watu akilenga kwa "popular art" - au Pop Art. Hapa aliona sawa kutumia picha za kila siku zilizokuwa mara nyingi matangazo ya kibiashara. Alichora chupa za Coca Cola na bidhaa nyingine. Kati ya picha mashuhuri ni ile ya kopo la supu ya nyanya ya Campbell Tomato Soup.

Katika chapa zake aliendelea kutumia picha za mazingira ya kila siku kutoka matangazo au magazeti akirudia sehemu ya picha tena na tena na kubadilisha rangi. Mfano ni chapo yaMarylin Monroe.

Mwanzoni watu hawakuelewa picha zake wakidai eti hii si sanaa lakini baada ya muda watu waliongezeka waliomwelewa na kumpenda.

Warhol alianza pia kupiga filamu fupifupi.


  • Chapa ya kopo la Campbell Tomato Soup 1964
    Chapa ya kopo la Campbell Tomato Soup 1964
  • Andy Warhol: Marilyn Monroe (1977)
    Andy Warhol: Marilyn Monroe (1977)
  • Tarakibu za Andy Warhol katika duka mjini Oslo 2007
    Tarakibu za Andy Warhol katika duka mjini Oslo 2007
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani wa Marekani bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuAndy Warhol kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Andy_Warhol&oldid=1274804"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp