Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Andalusia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Andalusia
Seville

Andalusia (kwaKihispania: Andalucía) ni jimbo la kujitawala (Kihisp.: comunidade autónoma) laHispania katikakusini yarasi ya Iberia.Mji mkuu niSevilla. Katikahistoria ni sehemu ya Hispania iliyowahi kutwaliwa na iliyotawaliwa kwakarne nyingi zaidi naWaarabuWaislamu.

Jiografia

[hariri |hariri chanzo]

Imepakana na majimbo ya Hispania yaExtremadura,Castilla-La Mancha naMurcia. Upande wamagharibi ikoUreno na upande wa kusini kuna pwani yaMediteranea,Mlango wa Gibraltar pamoja na eneo la Kiingereza laGibraltar na pwani yaAtlantiki.

Andalusia ina eneo lakm² 87,268 (17,2% ya Hispania yote) ambalo linakaliwa na watumilioni 8.

Mto mkubwa niGuadalquivir namlima mrefu niMulhacen (m 3,479).

Miji muhimu ni (idadi ya wakazi kwa mabano): Sevilla (705,000),Malaga (560,000),Cordoba,Granada,Almeria,Cadiz,Jaen,Huelva,Jerez naMarbella.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Andalusia ni eneo la pekee kutokana nahistoria yake. Iliwahi kutawaliwa na nchi za nje tangu zama za kale.Wafinisia walikuwa nakoloni hapa,Waroma wa Kale waliingiza eneo lote katikaDola la Roma wakifuatwa naWavandali halafu naWavisigothi waliojenga hapaufalme wao.

Mwaka711Waarabu naWaberber Waislamu walivamia Hispania kwa kuvuka mlango wa Gibraltar na kuanzishautawala wao katika sehemu kubwa zarasi ya Iberia uliokwisha mwaka1492. Kati ya maeneo yote ya Hispania ni Andalusia iliyokaa muda mrefu chini ya utawala wa Kiislamu. Eneo lote chini ya utawala wa Kiislamu likaitwa "Al-Andalus" na Andalusia ya leo ilikuwakiini chake.

Utamaduni wa Andalusia uliathiriwa sana na karne hizo chini yaUislamu. Cordoba ikawa kwa sehemu kubwa ya wakati ulemji mkuu wa utawala wa nchi ikawa mji mkubwa waUlaya.Vyuo vikuu vya Andalusia vikawa vitovu vyaelimu ambakowataalamu wa Ulaya,Afrika ya Kaskazini naAsia ya Magharibi walikutana. Hatauchumi ulistawi.

Kati ya mabaki ya kipindi hicho nimajengo kamaAlhambra wa Granada,majina ya kijiografia kama mto Guadalquivir (kutokaKiarabuالوادي الكبير "wadi al kabir" yaani mto mkubwa) namuziki wa Andalusia.

Utawala

[hariri |hariri chanzo]
Mikoa ya Andalusia.

Jimbo la Andalusia huwa na mikoa 8.Mahakama hufanya kazi kwenye msingi wa maeneo ya korti kwa jumla ni 125 katika Andalusia.

JimboMakao makuuWakaziDensitiIdadi ya manisipaaMaeneo ya korti
Almería
Almeria
635,850
72.5/km²
102
8
Cádiz
Cádiz
1,180,817
158.8/km²
44
14
Córdoba
Cordoba
788,287
72.4/km²
75
12
Granada
Granada
882,184
68.7/km²
168
9
Huelva
Huelva
483,792
47.7/km²
79
6
Jaén
Jaén
662,751
49.1/km²
97
10
Málaga
Málaga
1,491,287
204.1/km²
101
11
Seville
Seville
1,813,908
129.2/km²
105
15

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo yaHispania bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuAndalusia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Andalusia&oldid=1156104"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp