Mabata nindege wa maji wafamilia yaAnatidae wenyemadomo mafupi na mapana namiguu yenyengozi kati yavidole. Manyoya yao huwa na uwezo bora wa kufukuza maji kwa msaada wa mafuta maalumu. Mabata ndiyo moja ya familia za ndege ambazospishi zao zinauume, kwa sababu mabata wanapandana majini tu.
Mabata huchanganywa pengine na aina kadhaa za ndege wa maji wasiohusiana wenye maumbo yanayofanana, kamawazamaji,vibisi,kukuziwa nashaunge.
Mwili wote wa mabata kwa ujumla ni mrefu na mpana, na mabata wengi kwa wastani wanashingo fupi lakini shingo lamabata bukini namabata-maji ni ndefu. Umbo la mwili la mabata kwa kiasi fulani hutofautiana na hawa kwa kuwa kidogo wa duara kidogo. Miguu yenye magamba ni yenye nguvu na iliyokuwa vizuri, na kwa kawaida, na hurushwa nyuma kabisa ya mwili, hivyo zaidi hasa kwenye spishi za majini. Mbawa zake ni zenye nguvu na kwa ujumla ni ndogo na zilizochongoka, na kupaa kwa bata kunahitaji mapigo ya haraka bila ya kupumzika, hivyo kuhitaji misuli yenye nguvu sana. Hata hivyo spishi tatu za bata aina ya steamer hawawezi kuruka kabisa. Spishi nyingi za bata hushindwa kuruka vizuri kipindi cha kupukutisha manyoya ya zamani na kuotesha mapya; hutafuta mazingira salama yenye chakula kingi wakati huo. Hivyo basi kipindi hiki hufuata baada ya kipindi cha kuhama.
Ndege hawa wana rangi mbalimbali. Spishi kubwa hutafuta chakula aghalabu ardhini au kwa maji machache. Spishi ndogo nyingine hulamimea ya maji na huzamia kichwa chao tu, nyingine huzamia kabisa ili kukamatasamaki,wanyamakombe au mimea ya maji, lakini spishi kadhaa hutafuta chakula ardhini. Hujenga matago yao ardhini, juu ya mwamba, ndani ya shimo la miti au ndani ya pango lasungura,mhanga, k.y.k.
Manyoya ya spishi kadhaa hupendwa sana kama kijazo cha mito, mifarishi, mafuko ya kulalia na makoti. Spishi nyingi za mabata hutumika kama chakula.
Wataalamu hawakubaliana kuhusu uainisho wa mabata ndani ya familia yao. Kuna ainisho mbalimbali na mmoja tu unaonyeshwa hapa:
Spishi 27 za mabata wakubwa ndani ya jenasi 7 ambazo zinatokea kanda za halijoto wastani hasa kaskazini mwa ikweta lakini spishi chache kusini mwa ikweta (spishi kadhaa, kamabata-maji domo-fundo, zimewasilishwa kwa Afrika):
Jamii hii ya mabata makubwa wanaotokea mara nyingi nchini kavu ni kati yaAnserinae naAnatinae. Juzijuzi wataalamu wameainisha jenasi 10 na spishi 23 (moja imekwisha labda) ndani ya familia ndogo hii, nyingi zaidi kutoka kusini mwa ikweta:
Jamii ya mabata wazamaji ambao wantokea sehemu zote duniani ina spishi 16 ndani ya jenasi 3.Marmaronetta ilikuwa imeainishwa zamani miongoni mwa mabata wachovya lakini inaainishwa hapa sasa.
Netta (Mabata wazamaji, spishi 4, moja imekwisha yumkini)
Aythya (Mabata wazamaji, spishi 12, moja imekwisha yumkini)
Jamii ya moa-nalo (jina kwa Kihawaii) ni ya pekee. Mabata hawa walitokeaHawaii lakini wamekwisha sasa. Walikuwa wakubwa sana na domo nene sana na walifanana na mabata bukini ambao hawakuweza kuruka angani. Walikuwa na mnasaba na jenasiAnas.
Familia ndogo hii ina spishi 20 (moja au mbili zimekwisha). Spishi nyingi zaidi zinatokea kaskazini mwa ikweta, lakini kuna spishi mbili zaMergus kusini mwa ikweta.
Bata hula aina mbalimbali ya chakula kama vile kama vile nyasi, mimea ya majini, samaki, wadudu, amfibia wadogo, minyoo na moluski.Bata wanaoogelea na bata wa baharini wanakula wanyama chini kabisa ya kina cha maji. Ili kuweza kuzama kwa urahisi, bata wanaoogelea ni wazito kuliko bata aina ya dabbling, hivyo inakuwa vigumu kwa wao kuruka.Bata hawa wa dabbling hula kwenye uso wa maji au ardhini, au chini ya ardhi kwa kadiri ya uwezo atakaoweza kufikia bila ya kuzama kabisa.[4] Kuzunguka mdomo wa bata kuna umbo mithili ya kitana, iitwayopecten. Hii huchuja majimaji kwa kuyapitisha kwenye pande za mdomo na kubakiza chakula chochote ndani.Pecten pia hutumika kupuna manyoya.Baadhi ya spishi kama vilesmew,goosander namergansers wanauwezo wa kumeza samaki wakubwa.Bata wengine wana midomo bapa mahsusi kwa kazi za kuzoa na kuvuta kama vile kuvuta magugumaji, kuvuta minyoo na moluski nje ya matope, kutafuta lava wa wadudu, na kazi kubwa.
^ "Duckling". The American Heritage Dictionary of the English Language, Fourth Edition Copyright 2006 by Houghton Mifflin Company. Republished by dictionary.com,http://dictionary.reference.com/browse/duckling, Accessed 05-01-2008.
^ "Duckling". Kernerman English Multilingual Dictionary (Beta Version), 2000-2006 K Dictionaries Ltd., Republished by dictionary.com,http://dictionary.reference.com/browse/duckling, Accessed 05-01-2008.