Picha ya kuchonga kutokaJava inawaonyesha Buddha na Ananda
Ananda (karne ya 5 –4 KK) alikuwa mhudumu mkuu waBuddha na mmoja wa wanafunzi wake wakuu kumi. Miongoni mwa wanafunzi wengi wa Buddha, Ananda anaheshimiwa hasa kwa kuwa nakumbukumbu bora zaidi. Hivyo mafundisho mengi ya Buddha ambayo yamehifadhiwa katikamaandiko yaSutta-Piṭaka (Pāli; Sanskrit Sutra-Pitaka) yanategemea kukumbuka kwake. Kwa sababu hiyo, anaheshimiwa kamaMweka Hazina wa Dhamma, wakatiDhamma (Kisanskrit: dharma) inamaanisha mafundisho ya Buddha.
Sehemu yamapokeo inasema kwamba Ananda alikuwabinamu wa Buddha. Alitawazwa kuwamtawa na Puṇṇa Mantānīputta akawamwalimu wake. Baadaye Buddha alimchagua kuwa mhudumu wake.
Aliandamana na Buddha kwamaisha yake yote, akitenda sio tu kama msaidizi, bali piakatibu na msemaji wake.
Ānanda ni mmoja wa watu wanaopendwa sana katikaUbuddha. Alijulikana kwa kumbukumbu yake,elimu nahuruma, na mara nyingi alisifiwa na Buddha kwa mambo haya.