Amiri auEmir (ar. امير amīr autur. emir) ni cheo cha mtawala mwislamu anayesimamiaemirati. Kiasili maana yake ni "mwenye amri" kama cheo cha kijeshi au kiserikali.
Katika miaka ya kwanza ya Uislamu amiri alikuwa mkuu wa jeshi au sehemu ya jeshi. Baada ya kutwaa nchi alikuwa na nafasi kamagavana yakhalifa. Kutokana na upanuzi wa himaya ya kiislamu na ushaifu wa serikali kuu amiri aliweza kutawala mara nyingi kama mfalme mdogo lakini kwa kawaida alitafuta kibali cha khalifa.
amir al-mu’minin („mkuu wa waumini“) ilikuwa cheo cha heshima kwa makhalifa tangu Umar. Hadi leo ni cheo kimoja chasultani waMoroko.
amir al-umara’ („amiri wa maamiri“) ilikuwa cheo cha jemadari mkuu wa jeshi la Waabasiya. Baadaye katikaMilki ya Osmani ilikuwa cheo cha gavana wa jimbo kubwa.
amir al-bahr (امير البحر, „amiri wa bahari“) ilikuwa cheo cha kiongozi wa jeshi la maji ikaingia katika lugha za Kiulaya kama "admiral".
Nchi kadhaa zinazotumia jina "emirati" na cheo cha amiri kama mkuu wa dola ziko kwenye Bara Arabu. Mfano niKuwait naQatar. Pia nchi zilinazojulikana kwaKiswahili kamaFalme za Kiarabu zinajiita emirati chini ya maamiri.