Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Amerigo Vespucci

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Amerigo Vespucci

Amerigo Vespucci (Firenze,Italia,9 Machi1451 -Sevilla,Hispania,22 Februari1512) alikuwamfanyabiashara,nahodha nampelelezi kwenyepwani zaAmerika Kusini.Bara laAmerika limepokeajina kutoka kwake (Amerigo - Amerika).

Maisha

[hariri |hariri chanzo]

Mtoto wa tatu wamwanasheria wa Firenze, Amerigo alifanyakazi kwakampuni yaMedici akatumwa nayomwaka1491 kwendaSevilla katikaHispania. Huko alikutana naKolumbus amerudi kutokaAmerika.

Mwaka1499 alichukua nafasi yeye mwenyewe nakibali cha akina Medici akajiunga nasafari kwenda Amerika kufuata nyayo zasafari ya tatu ya Kolumbus kwa kusudi la kugundua zaidi ya pwani. Mbele ya pwani yaGuyana (leo:Surinam) aliachana na wenzake akaendeleakusini akafika hadimdomo wamto Amazonas akiamini ya kwamba amefikaUhindi jinsi ilivyokuwaimani ya kawaida wakati ule.

Katika safari yapili kwenda Amerika Kusini mwaka1501 /1502 alipitamwambao waBrazil naArgentina hadiPatagonia. Aliporudi aliamini ya kwamba nchi ng'ambo yaAtlantiki siAsia bali "dunia mpya" au bara jipya.Maandiko yake yalisambaa koteUlaya namwanajiografiaMjerumaniMartin Waldseemüller alitumia jina "Amerika" kwa heshima ya Amerigo alipochoraramani yake yadunia mwaka1507.

Upande wadini, alikuwaMkristo waKanisa Katoliki, tena mwanachama waUtawa wa Tatu wa Mt. Fransisko.

Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Amerigo_Vespucci&oldid=1007363"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp