Almere ni mji mdogo nchini Uholanzi: nyumba ya kwanza ilimalizika mnamo 1976, na Almere ikawa manispaa mnamo 1984. Ni manispaa kubwa sana katikaFlevoland ikiwa na idadi ya wakazi takriban 184,405 (7 Julai 2008)[1], na mji wa 8 kwa ukubwa nchiniUholanzi[2]. Mnamo mwezi wa Oktoba 2007, halmashauri ya jiji ya Almere imekubaliana na serikali kupanua mji na kufikia kuwa na wakazi wapatao 350,000 hadi ifikapo mwaka wa 2030.
Mipango ya awali yaIJsselmeerpolders aliona ardhi ikitumika kwa ajili ya kilimo. Hata hivyo, baada yaVita Kuu ya Pili ya Dunia ujenzi wa majumba ulihitajika kwa ukuzaji haraka wa idadi ya watu mjiniAmsterdam na miji miwili ilipangwa katika sehemu za ardhi ya Oostelijk Flevoland na Zuidelijk Flevoland. Mji katika eneo la Oostelijk Flevoland likawaLelystad. Mji katika eneo la Zuidelijk Flevoland uliendelea kuitaZuidweststad (Kiswahili: Mji wa Kusini Magharibi) katika hatua za mwanzoni, lakini katika miaka ya 1970 mji ukawaAlmere, umepewa jina baada ya jina la zama za kati laZuiderzee. Nyumba ya kwanza mjini Almere ilimalizwa mnamo 1976. Kwa kipind hicho mji bado ulikuwa ukimilikiwa naOpenbaar Lichaam Zuidelijke IJsselmeerpolders (Z.IJ.P.), ikiwa naLanddrost. Mnamo mwaka wa 1984 Almere ikapata kuwa manispaa rasmi. Awali, Almere ulitazamiwa kama mji wenye vituo kedekede. Wazo hili lilitelekezwa hapo baadaye kwa hisani ya kuwaruhusu majirani kama vile Tussen de Vaarten kujenga makazi yao mjini hapa. Pia kuna tofauti kadhaa katika mtindo wa ujenzi wa majumba ya sasa na yale ya zamani katika baadhi ya maeneo ya mji huu. Mpango wa ujenzi wa majumba ya mjini Almere kunako miaka ya 1970s ulikuwa wa pamoja na uliangalia sana hadhi ya usawa kijamii. Hata hivyo, kuanzia miaka ya 1990 majumba ya hali ya juu yalijengwa huku yakipishana na mfumo wa ujenzi (mfano kwenyeRegenboogbuurt).