Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Aljeria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Aljeria
الجمهورية الجزائرية الديمقراطية الشعبية (Kiarabu)
al-Jumhūriyah al-Jazāʾiriyah ad-Dīmuqrāṭiyah ash‑Shaʿbiyah
Kaulimbiu: بِالشَّعْبِ و لِلشَّعْبِ
"Biš-šaʿb wa liš-šaʿb"
"Kuwekwa na watu, kwa watu"
Wimbo wa taifa: قَسَمًا
Kasaman
"Tunaapa"
Mahali pa AljeriaMahali pa Aljeria
Ramani ya AljeriaRamani ya Aljeria
Mji mkuu
na mkubwa
Aljeri
36°42 N 3°13 E
Lugha rasmiKiarabu
Kiberiberi
Kabila85Waarabu
15Waberiberi
Dini99Wasuni (rasmi)
SerikaliJamhuri
  Rais
  Waziri Mkuu
  Rais wa Baraza
  Rais wa Bunge
Abdelmadjid Tebboune
Nadir Larbaoui
Salah Goudjil
Ibrahim Boughali
Idadi ya watu
  Kadirio la 202344 758 398[1]
PLT (PPP)Kadirio la 2023
  JumlaOngezeko USD bilioni 628.990[2]
  Kwa kila mtuOngezeko USD 13 681[2]
PLT (Kawaida)Kadirio la 2023
  JumlaOngezeko USD bilioni 224.107[2]
  Kwa kila mtuOngezeko USD 4 874[2]
HDI (2021)Ongezeko 0.745[3] -juu
SarafuDinari ya Aljeria
Majira ya saaUTC+1
Muundo wa tarehesiku/mwezi/mwaka
Upande wa magariKulia
Msimbo wa simu+213
Msimbo wa ISO 3166DZ
Jina la kikoa.dz

Aljeria , rasmi kamaJamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Aljeria ni nchi yaAfrika ya Kaskazini-Magharibi. Imepakana nabahari yaMediteranea,Moroko,Sahara ya Magharibi,Mauretania,Mali,Niger,Libya naTunisia. Aljeria ni nchi kubwa kuliko zote zaAfrika lakini sehemu kubwa ya eneo lake iko katikajangwa laSahara. Ina idadi ya watu takribani Milioni 46 ikiwa nchi ya 33 kubwa zaidi duniani kwa idadi ya watu.

Jina

[hariri |hariri chanzo]

Majina mengine yake ni: الجزائر,al-Jazā’ir (Kiarabu); الدزاير,al-dzāyīr (Kiarabu cha Aljeria); ⴷⵣⴰⵢⴻⵔ,Dzayer (Kiberiberi); Algérie (Kifaransa). Jina lake rasmi niJamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Aljeria (Kiarabu: الجمهورية الجزائرية الديمقراطية الشعبية,al-Jumhūriyah al-Jazāʾiriyah ad-Dīmuqrāṭiyah ash‑Shaʿbiyah;Kifaransa:République algérienne démocratique et populaire).

Asili ya jina

[hariri |hariri chanzo]

Jina la nchi limetokana namji mkuu Aljeri unaoitwa kwa jina lilelile kwa Kiarabual-Jazāʾir (الجزائر, "visiwa") linalohusu visiwa karibu na pwani yake. Aljeri iliitwa naBuluggin ibn Ziri.

Jiografia

[hariri |hariri chanzo]

Sehemu kubwa ya nchi nijangwa,Sahara iko upande wa kusini.Asilimia 20 za eneo la Aljeria upande wakaskazini ni makao kwa karibu wakazi wote. Maeneo haya nipwani yaMediteranea namilima ya Atlas. Atlas inapanda hadikimo chamita 2,308 juu yaUB.

Sahara inaanza kusini kwa Atlas na kanda yenyenyasi chache, halafu inafuata eneo la matuta yamchanga pasipomimea yote. Kusini kwake tena ninyanda za juu ambazo ni hasa maeneo yamiamba mitupu.

Kusini kabisa kuna milima kamaTassili n'Ajjer naAhaggar inayopanda hadi mita 2,918 na kuwa kama visiwa vya uoto katika jangwa.

Mito ya kudumu iko kaskazini tu, sehemu za pwani.Mabonde ya mito ya ndani ni makavu, isipokuwa baada yamvua mito mikali inajitokeza kwa masaa kadhaa.

Hali ya hewa

[hariri |hariri chanzo]

Kanda la kaskazini linahali ya hewa inayoathiriwa na Bahari ya Mediteranea. Hukohalijoto kwenyemweziAgosti ni 25°C na 12 °C wakati waJanuari.

Kwenye sehemu za juu kunabaridi na hatabarafu kwenyemajira ya Januari lakinijoto ni kali zaidi wakati wa Julai/Agosti.

Kusini ya Atlas inaanza hali ya hewa ya jangwani; halijoto inaweza kucheza zaidi ya 20 °C katika siku moja. Wakati wa joto halijoto inapita 40 °C lakini wakati wa baridi halijoto inashuka chini ya °C kwenye saa zausiku.

Mvua ni haba mno: kuna miaka mfululizo bilatone hata moja. Katika milima ya Ahaggar kunausimbishaji kidogo kutokana naukungu, kwa hiyomiti kadhaa namimea mingine iko.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Historia ya kale

[hariri |hariri chanzo]

Historia inayojulikana ilianza naWaberber ambao wametokana na mchanganyiko wa wakazi asilia.

Tangu mwaka1000 KKWafinisia walianza kufika na kujenga miji yao yabiashara kwenye pwani ya Mediteranea. Muhimu zaidi kati ya miji yao ulikuwaKarthago uliopanuautawala wake hadiHispania naGallia (Ufaransa ya Kusini).

Kumbe Waberber wa bara walijengamilki zao zaNumidia naMauretania.

Katikavita kati ya Karthago naRoma ya Kale Waberber walisimama upande waRoma, hivyo wakapatauhuru wao kwa muda kidogo, lakini wakati wakarne ya 1 KK Roma ilianza kutawala eneo la Aljeria moja kwa moja.

Numidia na Mauretania zilikuwa mashamba ya Roma na sehemu kubwa yanafaka zaItalia zililimwa huko.

Mawe yamaghofu ya miji ya kale bado yanaonyeshauhusiano wa Aljeria naDola la Roma lililoitawala kwakarne nyingi hadi kuja kwaWaarabu katikati yakarne ya 7.

Utawala wa Roma ulivurugika baada yaWavandali kutokaUlaya Kaskazini kufika na kuanzisha milki yao kwa muda wa karne moja.

Jeshi laKaisariJustiniani I waBizanti ilirudisha utawala wa Kiroma, ila tu katikakarne ya 7 uvamizi wa WaarabuWaislamu ulimaliza kipindi cha Kiroma.

Uvamizi wa Waarabu

[hariri |hariri chanzo]

Kuanzia mwaka642 vikosi vya Waislamu Waarabu kutokaMisri walishambulia eneo la Afrika ya Kaskazini. Mwanzoni hawakufaulu kuwashinda Wabizanti lakini, baada yauhamisho wa serikali ya makhalifa kutokaMedina kwendaDameski,Waumawiya walikazajitihada huko Afrika ya kaskazini.

Mwaka670jeshi kubwa la Waarabu likaunda mji waKairuan kusini yaTunis ya leo na mji huu ulikuwakitovu cha uenezaji. Walipoenea katika Aljeria ya leo walirudishwa na WaberberWakristo kwa msaada wa Wabizanti lakini jeshi lililofuata lilishinda na kufikia mwaka711 Afrika ya kaskazini yote (maana yake nchi za leo za Tunisia, Aljeria na Moroko) zilikuwa chini ya utawala wa Waarabu. Hapo sehemu kubwa ya Waberber walifanya haraka kujiunga na Uislamu wakasaidiana na Waarabu.

Matokeo hayo yalikuwa chanzo cha mabadiliko makubwa ya kudumu, maana yake upanuzi wa lugha ya Kiarabu kati ya wananchi na uenezaji wa Uislamu.

Ukoloni wa Wafaransa

[hariri |hariri chanzo]

Historia ya karibuni imeacha kumbukumbu yake inayoonekana katikaathira kubwa ya lugha nautamaduni waKifaransa kutokana naukoloni waUfaransa kati ya miaka1830 na1962.

Kwa Marais wa nchi tangu uhuru, angaliaOrodha ya Marais wa Aljeria.

Kwa sasa Aljeria inajenga upyaumoja wa kitaifa baada yavita ya wenyewe kwa wenyewe iliyoishia mwaka2002.

Nchi imebaki na idadi kubwa (25-30%) ya wakazi wakabila laWaberber ambao kihistoria ndio wakazi asilia. Lakini kwalugha,utamaduni nahistoria Aljeria ya leo ni sehemu ya dunia ya Kiarabu.

Wilaya za Aljeria

[hariri |hariri chanzo]

Kuna vitengo vya utawala 48 vinavyoitwawilaya, zinazolingana zaidi na mikoa katika nchi zingine.


1Adrar
2Chlef
3Laghouat
4Oum el-Bouaghi
5Batna
6Béjaïa
7Biskra
8Béchar
9Blida
10Bouira
11Tamanghasset
12Tébessa


13Tlemcen
14Tiaret
15Tizi Ouzou
16Aljeri
17Djelfa
18Jijel
19Sétif
20Saida
21Skikda
22Sidi Bel Abbes
23Annaba
24Guelma


25Constantine
26Médéa
27Mostaganem
28M'Sila
29Mascara
30Ouargla
31Oran
32El Bayadh
33Illizi
34Bordj Bou Arréridj
35Boumerdès
36El Tarf


37Tindouf
38Tissemsilt
39El Oued
40Khenchela
41Souk Ahras
42Tipasa
43Mila
44Aïn Defla
45Naama
46Aïn Témouchent
47Ghardaïa
48Relizane

Miji mikubwa

[hariri |hariri chanzo]

Watu

[hariri |hariri chanzo]

Wakazi wengi wana mchanganyiko wadamu ya Kiarabu na ya Kiberber na wachache ya Kituruki na ya Kiberber; karibu wote (98%) wanafuatadini yaUislamu.

Wakristo ni 1%, wakiwemoWaprotestanti naWakatoliki, lakini wengine wanashindwa kujitokeza kutokana nahofu yadhuluma.

Lugha rasmi ni Kiarabu (72%) na Kiberber (27-30%), lakini wengi sana wanaongea piaKifaransa.

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. "Angola".The World Factbook (kwa Kiingereza) (tol. la 2025).Shirika la Ujasusi la Marekani. Iliwekwa mnamo23 Machi 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) (Archived 2023 edition)
  2. 1234"World Economic Outlook Database, October 2023 Edition. (Algeria)".IMF.org.International Monetary Fund. 10 Oktoba 2023. Iliwekwa mnamo23 Machi 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Data Futures Exchange (Algeria)".data.undp.org.Umoja wa Mataifa. Iliwekwa mnamo23 Machi 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Marejeo mengine

[hariri |hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Serikali
Maelezo zaidi


Nchi zaAfrikaBara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) |Afrika Kusini |Algeria |Angola |Benin |Botswana |Burkina Faso |Burundi |Cabo Verde |Chad |Cote d'Ivoire |Eritrea |Eswatini |Ethiopia |Gabon |Gambia |Ghana |Guinea |Guinea Bisau |Guinea ya Ikweta |Jibuti |Kamerun |Kenya |Komori |Kongo (Jamhuri ya) |Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) |Lesotho |Liberia |Libya |Madagaska |Malawi |Mali |Misri |Morisi (Visiwa vya) |Mauritania |Moroko |Msumbiji |Namibia |Niger |Nigeria |Rwanda |Sahara ya Magharibi |Sao Tome na Principe |Senegal |Shelisheli |Sierra Leone |Somalia |Sudan |Sudan Kusini |Tanzania |Togo |Tunisia |Uganda |Zambia |Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje yaAfrika
Hispania:Kanari·Ceuta·Melilla |Italia:Pantelleria·Pelagie |Ufaransa:Mayotte·Réunion |Uingereza:·St. Helena·Diego Garcia |Ureno:Madeira
Nchi wanachama waUmoja wa Afrika (AU)
Makala hii kuhusu maeneo yaAlgeria bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuAljeria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Aljeria&oldid=1434001"
Jamii:
Jamii zilizofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp