Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Aljeri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Aljeri (Kiarabu:مدينة الجزائر,madīnat al-djazā'ir, "mji wa visiwa";Kifaransa:Alger) nimji mkuu pia mji mkubwa kabisa wa nchi yaAljeria ikiwa na wakazimilioni 2 (mwaka 2005), pamoja na mitaa ya nje takriban milioni 5. Ikomwambaoni mwabahari yaMediteranea.

Aljeri ni makao yaserikali nakitovu chauchumi,biashara,utamaduni namawasiliano nchini.

Kasbah yake imeorodheshwa naUNESCO kamaUrithi wa Dunia.

Waingereza walivamia meli za maharamia Aljeri mnamo Agosti 1816.
Majengo ya nyakati za ukoloni.
Mtaa wa Aljeri mwambaoni.
Uwanja wa "Mashahidi wa Uhuru".
Algiers inavyoonekana kutoka angani.
Aljeri inavyoonekana kutoka angani.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Mji ulianzishwa kamakoloni laWafinisia katikakarne ya 4 KK. Mahali palifaa kutokana na visiwa vinne vidogo vilivyokuwepo karibu na mwambao (lakini katikakarne ya 17BK viliunganishwa na bara).

Baada ya kuenea kwaDola la Roma ikawa mji wa Icosium na kuvamiwa naWaarabuWaislamu mwaka702.Waberber wakabila la Beni Mezghenna walikaa katika eneo hili. Mwaka960 kiongozi wa KiberberBuluggin ibn Ziri aliyekuwagavana wamakhalifa waFatimiya waMisri aliteua mahali pa Icosium na kujengaboma hapa. Mji uliitwa sasa "Al-djazair-Mezghenna" yaani "visiwa vya Beni Mezghenna". Ndiyoasili yajina la leo "Al djaza'ir (الجزائر)" yaani "visiwa".

Katikakarne zilizofuata mji ulivamiwa nawatawalaWamurabitun naWamuwahidun kutokaMoroko. Baadaye ukawa chini yamasultani wa Aljeria ya Kaskazini.

Mnamo mwaka1302Uhispania ilifaulu kushika visiwa vidogo mwambaoni kwa miaka kadhaa hadi kufukuzwa tena na mharamiaBarbarossa aliyeteka mji kwa niaba ya Sultani waUturuki.

Tangukarne ya 16 BK Aljeri ikawa mji wa kujitawala ndani yaDola la Uturuki. Imekuwa mara kwa maramakao makuu yamaharamia wa Mediteranea ya magharibi. Maharamia hao walishambuliajahazi zaWakristo kamaWaitalia,Wafaransa,Wahispania na kadhalika na kutekaabiria pamoja namabaharia. Waliuzwa kamawatumwa au kurudishwa kwao baada ya kulipiwapesa. Maharamia waliweza pia kushambulia miji ya Wakristo mwambaoni mwa Mediteranea na kutwaa wakazi kama watumwa. Hali hiyo ilisababisha tena na tena majaribio ya nchi zaUlaya kuvamia Aljeri lakini bila kufaulu hadikarne ya 19.

Mwaka1815Marekani ilishambulia Aljeri baada ya kupoteameli naraia kwa maharamia wa mji; mwaka1816Waingereza pamoja naWaholanzi walishambulia tena kwa kusudi la kulinda meli na raia zao. Walifaulu kumlazimisha mtawala wa Aljeri atiesahihimkataba wa kutochukua tena watumwa kutoka nchi za Ulaya ingawabiashara hii iliendelea kwa siri hata baadaye.

Mwaka1830 Wafaransa walivamia mji na kuanzisha utawala uliokuwa mwanzo wa ukoloni wa Kifaransa katika Aljeria.

Wafaransa walipanua na kubadilisha mji wa Kiarabu na Kiberber. Katika karne ya 19 Wafaransa wengi walihamia Aljeria hadi Aljeri ilikuwa mji mwenye wakazi wengi Wafaransa kuliko wenyeji waliokaa hasa katika mji wa kale ulioitwa "Kasbah". Wafaransa waliozaliwa Aljeria walijiita "pieds noir" (miguu myeusi).

Wakati waVita Kuu ya Pili ya Dunia Aljeria ilikuwa chini yaserikali ya Kifaransa katika maeneo yasiyovamiwa naUjerumani hadi kuingiliwa nawanajeshi Wamarekani na Waingereza mwaka1942. Baadaye ikawa mji mkuu wa "Ufaransa Huru" hadi mwisho wavita.

Tanguuhuru wa Aljeria (1962) Aljeri imekuwa mji mkuu wa Aljeria. Akina pieds noir walio wengi waliondoka wakihofia uchungu baada yavita vya ukombozi.

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo yaAlgeria bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuAljeri kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Aljeri&oldid=1324617"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp