[1]Alice Lakwena (pia:Alice Auma;1956 -17 Januari2007) alikuwakiongozi wa kiroho kati yaWaacholi waUganda aliyeanzishakundi la "Harakati ya Roho Mtakatifu" (Holy Spirit Movement) na kuendeshavita vya msituni dhidi yaserikali yaraisYoweri Museveni kuanziaAgosti1986 hadiNovemba1987.
Alizaliwa kwa jina la Alice Auma. Baada yandoambili zilizotengwa alikuwaMkatoliki.Tarehe25 Mei1985 alishikwa na mapepo akaonekana kamakichaa. Baada ya kupotea kwasiku40 akarudi kamamganga wa kienyeji akiwa na kipaji cha kuwasiliana namizimu kufuatana nautamaduni wa Kiacholi.
Pepo aliyesema mara nyingi kutoka mwake akajiita "Lakwena" na kutambulishwa kuwaroho yaafisa wa kijeshi waItalia.
Wakati wavita vya wenyewe kwa wenyewe wa 1986 nchini Uganda Alice alitangaza kwamba aliambiwa na Lakwena kuanzisha Harakati ya Roho Mtakatifu na kuwaita Waacholi wachukuesilaha kumalizavita na umwagaji wadamu.Wamisionari katika eneo walipewabarua iliyosema:
Akapata wafuasi na kushambuliajeshi la serikali akashinda mara kadhaa na kuwaongoza wafuasi wake kuelekeaKampala. Akawaambia waumini kwambarisasi hazitawadhuru, zitageuka kuwamaji tu. Baada ya kushindwa, kabla ya kufikiamji mkuu, Lakwena akaondoka kutoka katika Alice. Alice akakimbiliaKenya akakaa katikakambi la wakimbizi laDaadab.
Mdogo wakeJoseph Kony alikusanya baadaye mabaki yakikosi chake na kuunda kundi jipya la "Lord's Resistance Army".
Alice alifariki huko Daadabtarehe 17 Januari]2007 kutokana naugonjwa usioeleweka.