Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Alibaba Group

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Makao makuu ya kampuni ya Alibaba Group huko Hangzhou

Alibaba Group Holding Limited (pia hujulikana kamaAlibaba) nikampuni yateknolojia ya kimataifa yenye makao makuu yake nchiniChina iliyobobea katikabiashara ya mtandaoni na teknolojia .

Ilianzishwa mnamo28 Juni1999 hukoHangzhou,Zhejiang kampuni hiyo hutoa huduma za mauzo ya watumiaji kwa watumiaji (C2C), biashara kwa watumiaji (B2C), na biashara kwa biashara (B2B) kupitia lango zawavuti, pia hutoa huduma za malipo ya kielektroniki, injini za utaftaji wa ununuzi, na huduma zakompyuta ya wingu. Inamiliki na kuendesha matawi mengi ya kampuni ulimwenguni kote katika sekta nyingi za biashara.[1]

Mnamo19 Septemba2014, uwekezaji wa shea wa Alibaba (IPO) kwenye Soko lahisa laNew York ulikusanyadola za Kimarekani bilioni 25, na kuipa kampuni hiyo thamani ya soko la dola za Kimarekani bilioni 231. Hadi sasa IPO ni kubwa zaidi katikahistoria duniani.[2] Ni mojawapo ya mashirika 10 yenye thamani zaidi[3] na imetajwa kuwa kampuni ya 31 kwa ukubwa duniani kwenye orodha yaForbes Global 2000 mwaka2020.[4] MnamoJanuari2018, Alibaba ilikuwa kampuni ya pili katika bara laAsia kwa kuwa na thamani ya dola Kimarekani bilioni 500, baada ya mshindani wake kampuni ya Tencent.[5]

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. McClay, Rebecca (25 Julai 2017)."10 Companies Owned by Alibaba".Investopedia.Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Machi 2019. Iliwekwa mnamo3 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Baker, Lianna B.; Toonkel, Jessica; Vlastelica, Ryan (19 Septemba 2014). Orlofsky, Steve; Adler, Leslie (whr.)."Alibaba surges 38 percent on massive demand in market debut".Reuters.Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Februari 2019. Iliwekwa mnamo12 Oktoba 2017.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Beijing's battle to control its homegrown tech giants".Today. 24 Septemba 2017.Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Juni 2018. Iliwekwa mnamo19 Januari 2020.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Murphy, Andrea (13 Mei 2020)."Global 2000".Forbes.Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Desemba 2012. Iliwekwa mnamo27 Agosti 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. JAO, NICOLE (25 Januari 2018)."Alibaba market value hits the $500 billion valuation mark".TechNode.Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Mei 2019. Iliwekwa mnamo25 Januari 2018.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]


Makala hii kuhusu mambo yauchumi bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuAlibaba Group kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Alibaba_Group&oldid=1432123"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp