Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Alan Shepard

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alan Shepard mwezini

Alan Bartlett Shepard, Jr. (18 Novemba192321 Julai1998) alikuwa mtu wa pili aliyefika kwenyeanga-nje akiwamwanaanga wa kwanza waMarekani baada ya MrusiYuri Gagarin.

Alijiunga na wanamaji wa jeshi la Marekani akawa rubani na 1959 aliteuliwa kwa mradi wa kuandaa safari kwenda anga-nje. Wakati ule MArekani ilishindana na Umoja wa Kisovieti katika upelelezi wa anga -nje na Marekani ilitarajia kumpeleka mtu wa kwanza angani. Lakini matatizo ya kifundi yalichelewesha safari na Yuri Gagarin aliwatangulia12 Aprili1961.

Tarehe5 Mei1961 Shepard alirushwa kwa chombo chaMercury akafikia kimo cha kilomita 187 juu ya uso wa dunia akarudi baada ya dakika 15 na sekunde 22.

Mwaka 1969 aliingizwa katika mradi waApollo iliyoandaa safari za kufika mwezini. Alikuwa kiongozi wa safari ya Apollo 14 tar.31 Januari hadi9 Februari1971.

Alibeba kifaa chagolf pamoja na mipira yake akafaulu kupiga mpira wa golf kwenye uso wa mwezi.

Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Alan_Shepard&oldid=1049774"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp