Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Aktiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mstari wabuluu niDuara ya Aktiki; mstarimwekundu eneo la Aktiki kufuatana nahali ya hewa kuwa chini ya 10°C wakati waJulai.

Aktiki (pia:Aktika) ni sehemu yakaskazini kabisa yadunia yetu, ikijumlisha nchi nabahari inayozungukancha ya kaskazini. Sehemu za kaskazini zaUrusi,Alaska (Marekani),Kanada,Greenland (Udani),Skandinavia (Norwei,Uswidi naUfini) pamoja nabahari ya Aktiki huhesabiwa katika Aktiki.

Zote huwa nahali ya hewabaridimwaka wote.

Upande wakusini wa dunia kuna eneo linalolingana na hilo ambalo huitwaAntaktiki.

Tabia za Aktiki

[hariri |hariri chanzo]

Tabia kuu ya maeneo ya Aktiki ni baridi yake. Sehemu za karibu nancha za dunia ni baridi kwa sababu zinapokeamwanga wajua kwa muda wa nusu mwaka pekee na nusu nyingine kunagiza.Majira haya huitwa "usiku wa Aktiki" na "mchana wa Aktiki" na usiku au mchana hudumu miezi kadhaa.

Nchani kamili muda wamchana huu ni miezi sita na pia muda wausiku ni miezi sita. Kwa umbali fulani vipindi vyapambazuko vinaongezeka. Kwenye sehemu za kusini za Aktiki vipindi vya mchana ni virefu kuliko usiku, kwa hiyo kuna nafasi kwamimea kustawi inayolisha piawanyama mbalimbali.

Kutokana na baridi hiyo bahari ya Aktiki imeganda ikifunikwa naganda nene labarafu. Kwa hiyo sehemu za Aktiki hufunikwa na barafu tupu mwaka wote na hizi ni sehemu kubwa za Greenland zinazofunikwa nabarafuto, halafu Bahari ya Aktiki yenye ganda la barafu. Maeneo mengine yanatheluji, lakini theluji hii huyeyuka kwa vipindi vifupi vyajoto.

Ardhi imeganda pia yaanimaji naunyevu ndani ya ardhi hupatikana kama barafu tu na hii inafaya ardhi kuwa ngumu kamamwamba. Wakati wa vipindi vya joto kwenye mchana wa Aktikisentimita za juu za ardhi zinapoa na hiki ni kipindi cha mimea kuotea. Lakini chini ya uso wake ardhi bado imeganda na kwa sababu hiyo hakunamiti kwenye Aktikiː hakuna nafasi kwa ajili yamizizi yao.

Mipaka ya Aktiki

[hariri |hariri chanzo]

Hakuna mipaka ya Aktiki inayokubaliwa nawataalamu wote.

  • Mara nyingi watu humaanisha maeneo yote upande wa kaskazini wa "duara ya Aktiki" ambayo ni sawa nalatitudo wa 66° 33’N. Hii ni latitudo ambako kila mwaka mara moja jua linaonekanaangani kwa kipindi cha masaa 24 na vilevile mara moja jua halionekani kabisa kwa muda wa masaa 24. Kuelekea kaskazini ya hapa vipindi vya mchana na giza kabisa hurefuka hadi kufika nchani.
  • Wataalamu wengi hupendelea kuchora mpaka kufuatana na hali ya hewa halisi. Wanatumia kipimo cha halijoto ya wastani katika mwezi waJulai kuwa chini yasentigredi 10. Hii ni takriban sawa nampaka wa miti yaani hakuna miti tena ambako halijoto ni baridi zaidi.

Mimea

[hariri |hariri chanzo]

Kaskazini kabisa hakunamimea isipokuwaplankton baharini chini ya barafu. Penye barafu ya kudumu hakuna mimea. Sehemu za kaskazini kwenye nchi kavu ambako theluji huyeyuka kwa siku chache tu mimea ya pekee ni aina zakuvu nakuvumwani. Kusini zaidi kadiri jinsi baridi kali inavyopungua nafasi za mimea huongezeka. Kunamanyasi,majani mbalimbali na hatavichaka vinavyofikiakimo chamita 2 karibu na duara ya Aktiki.

Wanyama wa Aktiki

[hariri |hariri chanzo]

Mimea hii inalishamamalia kadhaa kama aina zasungura,panya,maksai maski aumbawala aktiki. Hao huvindwa na wanyama walanyama kama vilembweha aktiki nambwa mwitu. Kando ya bahari pale pasipoganda kuna mamalia wanaokamatasamaki kamasili na aina zanyangumi.Dubu aktiki huvinda wanyama wote wengine akipendelea sili na samaki.

Nje ya mamalia kunawadudu wengi wanaotokea kwenye kipindi cha joto pekee. Hao wanalisha piandege zinazokuja hapa wakati wa joto kwa kutagamayai na kuzaa wadogo wao. Ndege wengine wanaokamata samaki huishi kando ya bahari.

Kijiji cha nyumba za barafu za Waeskimo mnamo 1865
Familia ya Waeskimo wakikalia sleji

Watu

[hariri |hariri chanzo]

Kuna vikundi vya watu ambao wameishi katikamazingira ya Aktiki tangukarne nyingi. Wenyeji wa nchi za Aktiki niWaeskimo wanaoishi Greenland, Kanada, Alaska naSiberia (Urusi). Kiasili niwawindaji nawavuvi; walijenganyumba za barafu wakati wa baridi nahema kwenye kipindi cha joto, lakini siku hizi huishi katika nyumba za kawaida. Kwausafiri walitumiasleji zilizovutwa nambwa.

Vikundi vingine vilivyoingia katika nchi za Aktiki ni pamoja naWasami wa Skandinavia ya kaskazini na watu mbalimbali wa Siberia ya kaskazini ambao waliishi kama wawindaji auwafugaji wambawala aktiki.

Teknolojia ya kisasa imewezesha watu kutoka nje, kuhamia sehemu za Aktiki wanapofanyakazi kamawafanyabiashara, wachimbamadini,wanajeshi auwanasayansi wanaochungulia mazingira hii ya pekee. Ni hasa madini kama viledhahabu, mafuta yapetroli,makaa,shaba nachuma yaliyovuta watu wa nje kuja hapa.

Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Aktiki&oldid=959056"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp