Teknolojia ya akili mnemba inatumika kwa kiwango kikubwaviwandani,serikalini, na kwenyetafiti zakisayansi. Baadhi ya matumizi yenye wasifu mkubwa ya akili mnemba ni pamoja nainjini za utafutaji watovuti (kama ile yaGoogle), mifumo ya mapendekezo (inayotumika kwenyeprogramu tumishi zaYouTube,Tiktok,Amazon, naNetflix), kwenye utambuzi wahotuba za binadamu (kama Google Assistant, Siri na Alexa), kwenyemagari yanayojiendesha (kama Waymo), kwenyemifumo mikubwa ya lugha (inayotumika kwenyeroboti za mazungumzo kamaChatGPT na Gemini), kwenye mifumo ya uzalishaji picha kama DALL-E na michezo ya kimkakati (kama Chess na Go)[1].
Akili mnemba kamataaluma yasayansi ilianza rasmimwaka1956, neno "Akili mnemba" lilitungwa naJohn McCarthy, mwanasayansi wa kompyuta waMarekani katika mkutano wa kwanza wa Akili mnemba uliofanyika kwenye chuo cha Dartmouth[2].
Tafiti mbalimbali za akili mnemba zina malengo tofauti na hutumianjia tofauti kufikia malengo hayo. Malengo yaliyozoeleka ya tafiti ya akili mnemba ni pamoja naufikiriaji, uwasilishaji wa maarifa, upangaji, kujifunza,usindikaji wa lugha asili, utambuzi, na usaidizi waroboti.Akili ya jumla (uwezo wa kukamilisha kazi yoyote inayowezwa kufanywa na binadamu) ni moja kati ya malengo yamuda mrefu ya taaluma hii.
Wazo la mashine zinazofikiri linahistoria ndefu inayotanguliateknolojia ya kisasa. Mawazo ya awali kuhusu mashine zenye uwezo wa kufikiri au kuchukua maamuzi yalionekana katikafalsafa yaKigiriki, hadithi za kale, na baadaye maandiko yakarne ya 17 na18 kama yaGottfried Leibniz naThomas Hobbes waliodokeza kuwa fikra za kibinadamu zinaweza kueleweka kama mchakato wakihisabati. Hata hivyo, maendeleo halisi ya Akili Mnemba (AI) kama taaluma yakisayansi yalianza katikati yakarne ya 20.
Mwaka 1956 unachukuliwa kama mwanzo rasmi wa AI kama uwanja wa utafiti, kufuatia Mkutano wa Dartmouth uliowakutanisha wanasayansi kamaJohn McCarthy (aliyeasisi jina "Artificial Intelligence"),Marvin Minsky,Allen Newell, naHerbert Simon. Katika miaka ya 1950 na 60, AI ilizalisha matumaini makubwa, hukukompyuta za kwanza zikitengenezwa na programu zinazoweza kutatua matatizo yakihisabati au kucheza michezo kama chess. Hata hivyo, ukosefu wa uwezo wakompyuta na maarifa ya kutosha kuhusulugha na hisia za binadamu ulisababisha kipindi cha kusuasua katika maendeleo hayo kilichoitwa "AI winter."
Kuanzia miaka ya 1990 na kuendelea, AI ilianza kupata mafanikio mapya kwa msaada wa kompyuta zenye kasi zaidi, data kubwa (big data), na mbinu mpya kama machine learning na deep learning. Mafanikio makubwa kama ushindi wa kompyuta Deep Blue dhidi ya bingwa wa chess Garry Kasparov mwaka 1997, na baadaye mafanikio ya AlphaGo dhidi ya bingwa wa mchezo wa Go mwaka 2016, yalionyesha uwezo mkubwa wa AI. Katika karne ya 21, matumizi ya AI yameenea katika sekta kama afya, usafiri, mawasiliano, na huduma za kifedha, huku masuala ya kimaadili na usalama wa kiteknolojia yakichukua nafasi kubwa katika mijadala ya kisasa ya kisayansi na kijamii.
Makala hii kuhusu mambo yateknolojia bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.