Muziki ni mpangilio wasauti ili kuunda mseto wa umbo,utangamano, melodi, mdundo, au vilevile mbinu elezi. Muziki kwa ujumla unakubaliwa kuwa utamaduni wa ki-ulimwengu na hupatikana katika jamii zote za wanadamu.
Ufafanuzi wa muziki hutofautiana sana kifalsafa na kimbinu. Ingawa wasomi wanakubali kwamba muziki unafafanuliwa na vipengele maalum, hakuna makubaliano kuhusu uhakika wa vipengele hivi. Mara nyingi, muziki hutambulishwa kama mbinu ainati ya kuwasilisha ubunifu.[1]
Shughuli mbalimbali huhusika katika uundaji wa muziki, na mara nyingi hugawanywa katika kategoria za utunzi, ubunifu tendi na uigizaji. Muziki unaweza kuimbwa kwa kutumiaala mbalimbali za muziki, ikiwemo sauti ya binadamu. Inaweza pia kutungwa, kupangwa, au kuchezwa kifundi au kielektroniki, kama vile kisanduku muziki, paipu bareli, au programu dijitali kwenye kompyuta.
Aina ya muziki inayopatikana koteduniani ninyimbo ambazo ni maneno yanayotolewa kwa sauti na mahadhi fulani mara nyingi pamoja na ala za muziki. Kwa wanaorekodi sauti, wao huenda kwa studio kurekodi na huchukuliwa kwakinasasauti kilichoambatanishwa natarakilishi na kudhibitiwa nakompresa.
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuMuziki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.