Afrika nibara la pili kwa ukubwa na kwa idadi ya watuduniani, likiwa na eneo la takriban kilomita za mraba milioni 30.3 na kuwa na zaidi ya watu bilioni 1.4 kufikia mwaka 2024. Linapakana naBahari ya Mediteranea upande wa kaskazini,Bahari ya Atlantiki upande wa magharibi,Bahari ya Hindi upande wa kusini-mashariki, naBahari ya Shamu upande wa kaskazini-mashariki. Afrika ina mataifa 54 yanayotambuliwa kimataifa pamoja na maeneo kadhaa yenye viwango tofauti vya uhuru wa kiutawala.Bara hili lina utofauti mkubwa wa kijiografia, likijumuishaJangwa la Sahara,Mto Nile, Msitu wa mvua waKongo, Bonde Kuu la Ufa, naJangwa la Kalahari. Afrika inachukuliwa kuwa chimbuko la binadamu, ambapo ushahidi wa unaonyesha binadamu wa awali walitokea katika eneo hili mamilioni ya miaka iliyopita.
Afrika ina historia na urithi wa kitamaduni changamano, ulioundwa na ustaarabu wa kale kamaMisri,Karthago,Axum,Mali, naZimbabwe Kuu, pamoja na karne nyingi za biashara, uhamiaji, na ushawishi wa ukoloni. Mgawanyiko wa Afrika mwishoni mwa karne ya 19 ulisababisha utawala wa kikoloni waUlaya katika sehemu kubwa ya bara hili, huku mataifa mengi ya Afrika yakipata uhuru kati ya miaka ya 1950 na 1980.
Leo, Afrika ni bara linaloshuhudia mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kijamii, likiwa na rasilimali nyingi za asili, ongezeko la mijini, na mazingira mbalimbali ya kisiasa. Hata hivyo, linakabiliwa na changamoto kamaumaskini, ukosefu wa utulivu wa kisiasa, na matatizo ya kimazingira.
Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yaliitwa kwa jina la "Ethiopia" linalomaanisha nchi ya watu weusiweusi (kwaKigiriki "aithiops": aliyechomwa najua).
Katikaramani za kale kutokaUlaya maneno yote matatu ya "Afrika", "Lybia" na "Ethiopia" yanapatikana yakitumika kama jina la bara zima. Jina la "Afrika" limekuwa la kawaida kuanziakarne ya 16BK.
Jiografia
Afrika kutoka kwenyeMwezi (Ocktoba 2015)Uwiano kati ya Afrika, Asia na Amerika.
Afrika imezungukwa na bahari karibu pande zote. Kuna kiungo chembamba cha nchi kavu upande wakaskazinimashariki na bara la Asia kwenyerasi ya Sinai[4].
Barani kunanchi huru 54 zinazotambuliwa naUmoja wa Mataifa, maeneo 9 yenye hali ya pekee namadola mawili ambayo yanajitawala bila kutambuliwa kimataifa.
Wataalamu wengi wanakubaliana kutambua Afrika kama asili yabinadamu wote walioko duniani.[9]
Mwaka 2010 idadi ya wakazi wa nchi zote za Afrika ilipitabilioni 1. Ni kwambaidadi yao imeongezeka sana katika miaka 40 iliyopita, ikipiku zile zaUlaya naAmerika.
Ilhali mwaka1950 walikuwepo Waafrika milioni 229 pekee, idadi iliongezeka kuwa milioni 630 mwaka1990 na milioni 1200 mnamo2014.[10][11]
Hivyoasilimia yawatoto navijana ni kubwa. Kuna nchi kadhaa ambako zaidi yanusu ya wananchi wako chini yaumri wa miaka 25.[12] Wakazi wa Afrika ni vijana kuliko wale wa mabara mengine yote;[13][14] mwaka2012 umri wa wastani ulikuwa miaka 19.7, wakati kidunia ulikuwa 30.4.[15]
Waafrika wanaimani za dini nyingi tofauti, lakinitakwimu zinazotolewa hazina hakika, pia kwa sababu suala hilo ni nyeti kisiasa kwaserikali zenye mchanganyiko mkubwa wa watu, kama vileNigeria,Ethiopia naTanzania.[19][20]
Moore, Clark D., and Ann Dunbar (1968).Africa Yesterday and Today, in series,The George School Readings on Developing Lands. New York: Praeger Publishers.