Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Afghanistan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
د افغانستان اسلامي امارت
Də Afġānistān Islāmī Imārat
امارت اسلامی افغانستان
Imārat-i Islāmī-yi Afğānistān

Emirati ya Kiislamu ya Afghanistan
Bendera ya AfghanistanNembo ya Afghanistan
BenderaNembo
Kaulimbiu ya taifa:لا إله إلا الله، محمد رسول الله (Shahada)
Lā ilāhā illā-llāhu; muhammadun rasūlu-llāhi
("Hakuna mungu ilaAllah;Muhammad ni mtume wa Allah")
Wimbo wa taifa:Dā Də Bātorāno Kor
Lokeshen ya Afghanistan
Mji mkuuKabul
34°31′ N 69°08′ E
Mji mkubwa nchiniKabul
Lugha rasmiKipashto,Kifarsi
SerikaliUtheokrasi wakidikteta chini yaemirati ya Kiislamu
Hibatullah Akhundzada
Hasan Akhund
Uhuru
Tarehe
KutokaUingereza
19 Agosti1919
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
652,864 km² (41)
N/A
Idadi ya watu
 -2015 kadirio
 -1979 sensa
 - Msongamano wa watu
 
32,564,342 (40th)
13,051,358
43.5/km² (150th)
FedhaAfghani(Af) (AFN)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+4:30)
(UTC+4:30)
Intaneti TLD.af
Kodi ya simu+93

-



Afghanistan (jina rasmi:Emirati ya Kiislamu ya Afghanistan) ni nchi yabara laAsia. Inapakana na nchi zaPakistan,Uajemi,Turkmenistan,Usbekistan,Tajikistan naChina.

Ni nchi yamilima mirefu mingi inayofunika 3/4 za uso wake. Kutokana na tabia ya nchi wakazi wengi huishi katika jumuiya za kikabila.

Mji mkuu niKabul.

Jiografia

Afghanistan ni nchi bilapwani kwenyebahari yoyote. Sehemu kubwa ya eneo lake lenyekm² 652,090 nimilima.Asilimia 90 za nchi ikomita 600 au zaidi juu yaUB ikiendelea kupanda hadi mita 7,485 kwenye ncha yamlima Noshak. Safu za milima kubwa niHindu Kush naPamir.

Katika kaskazini na kusini magharibi kuna maeneo ya tambarare yenye tabia yajangwa. Maeneo makubwa niyabisi na nusu jangwa au jangwa. Sehemu za milima zinapokeamvua natheluji, lakinimito mingi inayoanzia huko inapelekamaji yake nje ya nchi, kwenda Iran, Pakistan na Turkmenistan.

Hali ya hewa inategemea mahali nakimo. Sehemu za juu milimani huwa najalidi kali wakati wa majira yakipupwe na tambarare za chini huwa najoto kali wakati wamajira ya joto.

MjiHalijoto ya mchana/usiku mwezi wa JanuariHalijoto ya mchana/usiku mwezi wa Julai
Herat9 °C/-3 °C37 °C/21 °C
Kabul5 °C/-7 °C32 °C/15 °C
Kandahar12 °C/0 °C40 °C/23 °C

Historia

Kabla yakarne ya 19 nchi yote au sehemu mbalimbali zilikuwa chini yamilki jirani, hata kama sehemu za eneo la Afghanistan zilijitegemea chini ya watawala wadogo. Kwa vipindi virefu vyahistoria Afghanistan ilikuwa sehemu yamilki zaUajemi (Iran).

Afghanistan kama nchi ya pekee ilianza kutokea katikakarne ya 18, watawala wa kieneo walipojiondoa katika himaya ya Uajemi.

Nchi ilifaulu kutunzauhuru wake kutokana na mashindano yaUingereza naUrusi pamoja na nguvu na ukali wa wapiganaji kutokamakabila yake. Watawala wa kwanza waliofaulu kuunganisha sehemu nyingi za nchi chini yamamlaka yao walitawala kamaEmir, na tangumwaka1926 kwacheo chamfalme.

MfalmeZahir Shah alipinduliwa mwaka1973 na nchi ikawa Jamhuri. Mnamo1978wanajeshiWakomunisti walipinduaserikali na kutangaza serikali ya kisoshalisti iliyoanzisha mabadiliko mengi katikajamii kama ugawaji mpya wamashamba,shule zilizounganishawasichana nawavulana na kukamatwa kwaviongozi wadini waliopinga maazimio ya serikali. Mabadiliko hayo yalileta upinzani kutokawanamgambo waliopigana najeshi la serikali.

Mnamo Disemba1979Umoja wa Kisovyeti iliamua kuingilia kati ikavamia nchi kwa shabaha ya kuokoa utawala wa Wakomunisti, lakini ukapaswa kujiondoa tena mwaka1989.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilifuata kati ya vikundi vya wapinzani ambako nchi jirani yaPakistan ilikuwa na athira kubwa kwa kutumasilaha napesa. Nchi ilikuwa tena na kipindi kifupi chaserikali ya kitaifa, lakini vita vya wenyewe kwa wenyewe viliendelea katika sehemu za nchi.

Mateso ya vita hivyo yalihamasishawalimu nawanafunzi wamadrasa (shule zaKiislamu) kuchukua silaha dhidi ya migambo mbalimbali na kuwashinda wakijulikana kwa jina laTaliban (jina linamaanisha wanafunzi wa madrasa). Taliban walifaulu kutekaKabul kwa msaada kutokaSaudia na Pakistan mwaka1996. Walitangaza Emirati ya Kiislamu ya Afghanistan wakanzisha utawala uliotumia mafundisho makali yasharia ya Kiislamu. Utawala wao ulikuwa maarufu kwa kuzuia wanawake wasishiriki katikamaisha ya hadharani, kuwalazimisha kuvaaburka, kufunga shule za wasichana, kukatazakazi kwa wanawake nje yanyumba zao tena matumizi yaadhabu kali kama kukatamkono wamwizi na kumwuamzinzi kwa kumpigamawe.

Serikali ya Taliban ilikwisha kwa sababu walimruhusuOsama bin Laden pamoja nakundi lake laAl-Qaida kuwa na kimbilio nchini. Baada yaShambulio la 11 Septemba 2001Marekani ililipakisasi kwa kushambulia Afghanistan.

Hali ya vita iliendelea ndani ya Afghanistan katika vita vya Marekani naNATO2001-2014. Tangu Disemba 2014 nchi za NATO zilitangaza ya kwamba wamemaliza kushiriki mapigano na kuondoa sehemu kubwa yawanajeshi kutoka Afghanistan. Vikosi vya NATO vimebakizwa kwa shabaha ya kusaidia jeshi la kitaifa.

Mnamo mwaka2020 Marekani ilipatana na Taliban kwamba Marekani ingeondoaaskari wote kutoka Afghanistan katika mwaka 2021. Taliban waliahidi kutoshambulia wanajeshi wa Marekani lakini waliongeza mashambulio yao dhidi ya jeshi la serikali.

Baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa NATO na idadi kubwa ya Wamarekani, Taliban walianza kuvamia maeneo mengi ilhali nguvu ya jeshi la kitaifa liliporomoka. Mnamo15 Agosti 2021, rais wa Afghanistan aliondoka nchini na Taliban waliteka tena Kabul.

Baada ya kutwaa Kabul, wasemaji wa Taliban walitangaza kwamba wanataka kufuatasiasa tofauti kiasi na ile ya zamani. Wasemaji walidai kwamba wataruhusu wanawake kufanya kazi na wasichana kusoma, kama wanakubali kuvaahijabu. Walitangaza pia kwamba watasamehe wananchi wote waliowahi kupigana nao. Hata hivyo, Waafghanistan wengi walijaribu kukimbia nchi kwa njia mbalimbali.

Mwisho wa Agosti 2021, Taliban walidhibiti nchi yote isipokuwa jimbo laPanjshir, ambapo wapinzani walijipanga chini ya makamu wa rais aliyejitangaza kuwarais kufuatana nakatiba ya jamhuri.

Watu

Mwaka2015 wakazi walikadiriwa kuwa 32,564,342, wakiwemo wakimbizimilioni 2.5 wanaoishi Pakistan na Iran.

Kwa kuwa nchi iko kwenye njia zinazounganisha maeneo mbalimbali ya Asia, wakazi hao ni mchanganyiko mkuuːkabila kubwa ni laWapashtuni (42%), halafu kunaWatajiki (27%),Wauzbeki (9%),Wahazara (8%) n.k.

Wengi wanaongea zaidi yalugha moja (angaliaorodha ya lugha za Afghanistan).Zile rasmi niKipashto (35%) naKidari (50%), ambazo zote mbili ni za jamii yaKiajemi kati yaLugha za Kihindi-Kiulaya.

Upande wadini, zaidi ya 99% niWaislamu (90%Wasuni, 7%Washia n.k.). Ndiyodini rasmi. Waliobaki niWazoroasta,Wakristo,Wahindu,Singasinga n.k.

Tazama pia

Kujisomea

Vitabu
Makala
  • Meek, James.Worse than a Defeat. London Review of Books, Vol. 36, No. 24, December 2014, pages 3–10

Viungo vya nje

Nchi na maeneo yaAsia

Afghanistan |Armenia2 |Azerbaijan |Bahrain |Bangladesh |Bhutan |Brunei |China |Falme za Kiarabu |Georgia2 |Hong Kong3 |Indonesia |Iraq |Israel |Jamhuri ya China (Taiwan) |Japani |Kamboja |Kazakhstan |Kirgizia |Korea Kaskazini |Korea Kusini |Kupro2 |Kuwait |Laos |Lebanoni |Macau3 |Malaysia |Maldivi |Mongolia |Myanmar |Nepal |Omani |Pakistan |Palestina |Qatar |Saudia |Singapuri |Sri Lanka |Syria |Tajikistan |Timor ya Mashariki |Turkmenistan |Uajemi |Ufilipino |Uhindi |Urusi1 |Uthai |Uturuki1 |Uzbekistan |Vietnam |Yemen |Yordani

1. Nchi ina maeneo katikaAsia naUlaya. 2. Nchi ikoAsia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi zaUlaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo yaAsia bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuAfghanistan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Afghanistan&oldid=1339773"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp