Mara ya kwanza Akinnuoye-Agbaje alionekana kwenye televisheni ni kwa nyimbo yaMary J. Blige inayoitwa "Love No Limit" mnamo mwaka 1993. Muda huo huo, alionekana katika video yaPet Shop Boys kwenye nyimbo yao ya"Jealousy" ambapo aliigiza kama mzinifu.
Yeye anafahamika kwa kuigiza kamaSimon Adebisi kwenye kipindi kilichoigizwa gerezani chaOzkwenye stesheni ya HBO, na kwenye kipindi chaLost kamaEko inayoonyeshwa kwenye stesheni yaABC. Yeye ameigiza katika filamu kadhaa tangu alipoanza mnamo mwaka 1994 na ameigiza katika filamu za kujulikana kamaThe Bourne Identity, ambapo yeye ni dikteta wa Afrika, na kama Lock-Nah katika filamu yaThe Mummy Returns, naHeavy Duty katika [2].Yeye pia alisema kuwa atakuwa akingoza filamu inayohadithia kuhusu maisha yake.Siku ya Ijumaa 14 Agosti 2009 Adewale aliigiza katika onyesho la pili, msimu wa 8 kwenye kipindi chaMonk.
Akinnuoye-Agbaje ni wa dini yaBuddha.[1]
Yeye alikamatwa mjiniHonolulu, Hawaii tarehe 2 Septemba 2006 kwa kutomtii afisa wa polisi na kuendesha gari bila leseni. Yeye alitolewa baada ya masaa sita[2] kwa dhamana ya$ 500.[3] Mnamo 26 Septemba 2006, yeye alifutiwa mashtaka yote baada ya kutoa ushahidi kwamba alikuwa na leseni.
Akinnuoye-Agbaje aliomba kutolewa kwenye kipindi chaLost, akiongelea hamu ya kurudi mjini London baada ya wazazi wake kufariki na azma yake ya kuongoza filamu huko.[4]