Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Abu Bakr

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Abu Bakr jinsi alivyomlinda mtume Muhammad dhidi ya watu wa Maka waliotaka kumtupia mawe -mchoro wakarne ya 16 -Uturuki.

Abu Bakr (kwaKar.: أبو بكر‎‎Abū Bakr al-Ṣiddīq;Makka,573 kwa jina la ʿAbd Allah;Madina,23 Agosti634) alikuwakhalifa wa kwanza katikaUislamu baada yakifo chaMtume Muhammad. Alikuwababa waAisha,mke mdogo waMuhammad.

Abu Bakr alikuwa kati ya wafuasi wa Mtume Muhammad walioshikamana naye tangu mwanzo na kuongozana naye wakati wahijra.

Baada ya kifo cha mtume huyo alichaguliwa kuwakiongozi mpya kwa msaada waUmar ibn al-Khattab naWakuraish. Abu Bakr akatumiacheo cha "mfuasi wa mtume waAllah" (khalifatu-rasuli-llah) au khalifa.

Kati ya kazi zake za kwanza ilikuwavita za riddah dhidi yamakabila yaWaarabu walioona ya kwamba baada ya kifo cha Muhammad hawakuwa nawajibu kwa kiongozi mpya. Wengine walikataa malipo yazakat, wengine walirudiadini zao za awali.

Baada ya kushindavita hizi Abu Bakr alitumajeshi lake dhidi yaBizanti naUajemi. Hapokaskazini Waarabu walikutana namilki mbili kubwa zilizochoka baada ya vita ya mnamo mwaka wa 30 kati yao. Zaidi ya hapo Wajemi walikuwa katika kipindi chavita ya wenyewe kwa wenyewe.JemadariKhalid bin Walid alishambuliaHira katikaMesopotamia na upande wa Bizanti jeshi la Waarabu likaingia katikaPalestina.

Kwa upande wadini Abu Bakr alimpaUmar bin Khattab kazi ya kukusanya mapokeo yaKorani. Kabla ya kuagadunia alimtaja Umar kamamwandamizi wake.Alifariki mjiniMadinamnamo mwaka634 akazikwa kando ya Muhammad katikaMasjid al Nabawi.

Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Abu_Bakr&oldid=1234120"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp