Mary Todd Lincoln (m.1842) «start:(1842-11-04)»"Marriage: Mary Todd Lincoln to Abraham Lincoln"Location:(linkback://sw.wikipedia.org/wiki/Abraham_Lincoln)
watoto
Robert Todd Lincoln Edward Baker Lincoln William Wallace Lincoln Tad Lincoln
Lincoln alipinga utumwa lakini kwaasili hakuwa mpinzani mkali; aliona kwamba utumwa uliwahi kukubaliwa katikakatiba ya Marekani tangu mwanzo lakini aliona hali hiyo iendelee katika majimbo ya kusini tu yaliyokuwa sehemu za Marekani tangu mwanzo ilhali majimbo ya kaskazini yaliukataa. Alipinga upanuzi wa utumwa katika majimbo mapya yaliyoendelea kuundwa wakatiMuungano wa Madola ya Amerika ulipanua eneo lake upande wamagharibi na kuelekeautawala juu ya nchi yote kati yaKanada naMeksiko.
Alipinga hatua yamajimbo ya kusini kujitenga na baada ya mashambulio dhidi ya vituo vya kijeshi vyaMuungano aliamua kuchukua hatua za kijeshi ili kurudisha majimbo yaliyoasi. Mwanzoni mwavita alitangaza nia yake haikuwa kumaliza utumwa kusini; lakini baada ya vita kuendelea miaka miwili alikuwa tayari kuchuka hatua kali zaidi.
Mwaka1862 alitiasahihi tangazo la Bunge la Muungano kuwa watumwa wote waliomilikiwa naaskari waliopiga vita dhidi ya Muungano wakamatwe na kutangazwa huru. Mwisho wa 1862 Lincoln mwenyewe alitoaamri ya kutangazauhuru wa watumwa wote katika majimbo yote yaliyotumiasilaha dhidi ya Muungano. Alikubali pia kuajiri watumwa kuwawanajeshi kama wamekimbia kutoka upande wa kusini na kujitolea. Hakufuta kabisa utumwa kwa sababu bado kulikuwa na majimbo machache yenye utumwa yaliyobaki katika Muungano. Baada ya mwisho wa vita Lincoln alipata kibali cha bunge cha kufuta utumwa kabisa katika maeneo yote ya Marekani.