Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

A

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alfabeti ya Kilatini
AaBbCcDd
EeFfGgHhIiJj
KkLlMmNnOoPp
QqRrSsTtUuVv
WwXxYyZz
(Kwa matumizi ya Kiswahili)
chdhghkh
mbmvndngng'nj
nynzshth
HerufiA kwa mwandishi mbalimbali

A ni herufi ya kwanza katikaalfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko waKiswahili cha kisasa. Asili yake niAlfa yaKigiriki.

Maana za A

  • katikamuzikiA ni noti.
  • KatikatibaA ni aina yadamu.
  • Kwa magariA ni alama ya gari kutokaAustria.
  • Kati ya vipimoa ni alama yaAr yaani eneo la mita kumi mara kumi
  • KatikafizikiaA ni alama yaampea.
  • Katika shule za nchi mbalimbaliA nidaraja la juu i(la kufaulu) linalowezekana
  • kwa maana ya kiashirioA ni alama ya chanzo

Historia

Kichwa ch ng'ombe
(Alama ya kale iliyokuwa silabi)
"Alef" ya Wafinisia
(neno lao kwa ng'ombe)
Kigiriki
Alfa
Kilatini
A
Proto-semitic ox headPhoenician alephGreek alphaRoman A

Asili ya herufi A ni miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia.

Kama herufi nyingine za alfabeti ya Kigiriki alfa imetoka katikaalfabeti ya Wafinisia iliyokuwaalfabeti ya kwanza ya dunia. Wafinisia waliendelezamwandiko wa kikabari wa kale uliokuwa mwandiko wa silabi na kuifanya alfabeti ya herufi moja-moja.

Faida ya alfabeti ni ya kwamba inahitaji alama chache kulingana na mwandiko wa silabi mwenye alama kwa kila silabi ya lugha fulani au mwandiko picha unaohitaji maelfu ya alama za picha.

Alef ya Wafinisia

Wafinisia walichukua alama ya ng'ombe wakairahisisha na kuiita kwa neno lao "alef" lenye maana ya "ng'ombe" lakini walisoma tu "'" yaani kituo kimya jinsi ilivyo hadi sasa katika alef yaKiebrania. Hivyo walifanya picha kuwa herufi. Herufi ilinama jinsi kichwa cha ng'ombe kinavyoonekana kikitazamiwa kutoka kando.

Alfa ya Wagiriki

Wagiriki walipokea alfabeti kutoka Wafinisia na pia jina la herufi hii. Hawakuwa na matumizi kwa ile sauti kimya ya Wafinisia lakini walihitaji herufi za vokali ambazo hazikuandikwa katika Kifinisia jinsi ilivyo hadi sasa katika Kiebrania na pia mara nyingi katikaKiarabu.

Kwa hiyo walitumia alama kwa sauti ya A wakabadilisha kidogo jina kuwa "alfa" badala ya "alef". Lakini katika lugha yao hawakuelewa tena maana asilia iliyokuwa "ng'ombe". Kwao ilikuwa alama ya sauti tu.

Mwanzoni waliandika herufi kwa umbo la kulala kama Wafinisia lakini katika karne za baadaye herufi iligeuzwa na kuandikwa mwishowe jinsi tunavyozoea leo.

Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=A&oldid=1241440"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp