50 Cent alizaliwa mjiniSouth Jamaica, Queens ndani yaNew York,Marekani.50 Cent ameanza kujishughulisha na masuala ya uuzaji wa dawa za kulevya toka akiwa na umri wa miaka 12, hiyo ilikuwa kwenye miaka ya '80', akiwa anajushughulisha na masuala ya uuzaji wa dawa za kulevya. 50 Cent pia akawa anajaribu kidogo masuala ya muziki wa rap na hip hop.
50 Cent alipigwa risasi tisa mnamomwaka2000. Kadri miaka inavyozidi kwenda 50 Cent akabahatika kutoa tepu ya nyimbo mchanganyiko ilyokuwa inaitwa "Guess Who's Back?" mnamomwaka wa2002.
50 Cent aligunduliwa kipaji chake na mwanamuziki 'Eminem' na kumwingiza katika studio yaInterscope Records kwa msaada waEminem naDr. Dre, ambaye ndiye aliye tayarisha albamu ya kwanza ya 50 Cent na kumpa mafanikio makubwa katika ulimwengu wa muziki.