Kila mtu anaweza kuhariri makala yoyote, kutoa makosa ya lugha, kutohoa maneno na kuendeleza na kukuza makala, kwa kuandika kwa ufupi au kwa urefu. Tunakushauri ujiandikishe nakufungua akaunti. AngaliaWikipedia:Mwongozo ili ujifunze unavyoweza kuhariri au kusanifisha ukurasa. Usisite kushiriki; kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano, na hautaisha kamwe. Kamusi elezo itaimarika vizuri zaidi kila wakati. Angaliaukurasa wa jumuia,ukurasa wa jamii, na ule wamakala za msingi za kamusi elezo ili kung'amua unaweza kufanya kazi zipi ili kuboresha Wikipedia.
Papa Yohane Paulo II (kwaKilatini:Ioannes Paulus PP. II; kwaKiitalia:Giovanni Paolo II; kwaKipolandi:Jan Paweł II; kwaKiingereza:John Paul II;18 Mei1920 -2 Aprili2005) alikuwa Papa wa 264 kuanzia tarehe 16 Oktoba 1978 hadi kifo chake akidumu katika huduma hiyo kirefu kuliko Mapapa wengine wote, isipokuwa Mtume Petro na Papa Pius IX. AlitokeaWadowice,Krakow,Polandi.
Alimfuata Papa Yohane Paulo I akiwa Papa wa kwanza asiye Mwitalia tangu miaka 455 iliyopita, wakati wa Mholanzi Papa Adrian VI (1522 - 1523), tena Papa wa kwanza kutoka Polandi (na makabila yoyote ya Waslavi) katika historia ya Kanisa. Alifuatwa na Papa Benedikto XVI.
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Karol Józef Wojtyła (matamshi: ˈkarɔl ˈjuzɛf vɔiˈtɨwa).
Wengi wanamhesabu kati ya watu walioathiri zaidi karne ya 20, hasa kwa sababu tangu mwanzo wa Upapa wake alipambana na Ukomunisti uliotesa nchi yake asili na nyinginezo, akachangia kwa kiasi kikubwa kikomo chake na kusambaratika kwa Urusi.
Vilevile alilaumu ubepari wa nchi za magharibi na kudai haki katika jamii zote, akitetea hasa uhai wa binadamu na uhuru wa dini.
Upande wa dini, aliboresha uhusiano kati ya Kanisa Katoliki na madhehebu mengine ya Ukristo[11] pamoja na ule na dini mbalimbali, kuanzia Uyahudi, Ubudha, Uislamu.
Ziara zake 104 kati nchi 129 ulimwenguni kote, mbali na 146 nchini Italia na 317 katika parokia za Roma, zilikusanya mara nyingi umati mkubwa (hadi zaidi ya milioni 4 huko Manila, Ufilipino, mwishoni mwa siku ya kimataifa ya vijana), na kumfanya asafiri kuliko jumla ya mapapa wote waliomtangulia, akiwa mmojawapo kati ya viongozi wa dunia waliosafiri zaidi.
Papa Wojtyła alitangaza wenye heri 1,340 na watakatifu 483, ili kuwapa Wakristo wa leo vielelezo mbalimbali kwa maisha yao ili walenge utakatifu walioitiwa na Mungu. Idadi hiyo ni kubwa kuliko ile ya waliotangazwa na jumla ya Mapapa wote waliomtangulia walau katika karne tano za mwisho.
Alikuwa anaongea lugha mbalimbali, zikiwemo za Kipolandi, Kiitalia, Kifaransa, Kijerumani, Kiingereza, Kihispania, Kireno, Kiukraina, Kirusi, Kiserbokroatia, Kiesperanto, Kilatini na Kigiriki cha kale.
Yohane Paulo II alitangazwa na mwandamizi wake Papa Benedikto XVI kuwa mwenye heri tarehe 1 Mei 2011, halafu Papa Fransisko akamtangaza mtakatifu tarehe 27 Aprili 2014.
Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 22 Oktoba[26], kulingana na siku ya kuanza rasmi huduma yake ya Kipapa kwa Misa iliyofanyika katika uwanja mbele ya Basilika la Mt. Petro,Vatikani.►Soma zaidi
Picha nzuri ya wiki
Ziara ya Mwalimu Nyerere wa Tanzania mnamo Machi 12, 1985; Rais Nyerere akisikiliza maswali.
Julius Nyerere (Butiama, 13 Aprili 1922 - London, 14 Oktoba 1999) alikuwa Rais wa kwanza wa Tanzania na Baba wa Taifa. Aliongoza Tanganyika tangu uhuru mwaka 1961 kama Waziri Mkuu, kisha baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964, aliongoza Tanzania kama Rais hadi 1985. Aliundasera ya Ujamaa na Kujitegemea ambayo iliweka msisitizo kwenye usawa wa kijamii, elimu kwa wote na umoja wa kitaifa. Baada ya kustaafu urais, aliendelea kuishi kwa kuendeleza shughuli za kijamii na kilimo, na alifariki dunia kutokana na saratani ya damu tarehe 14 Oktoba 1999 akiwa London, na kuzikwa Butiama. Je ungependa kusoma zaidi kuhusu Mtu huyu? au ungependa kuchangia zaidi kuhusu mtu huyu? funguaHapa
Takwimu ya Wikipedia ya Kiswahili
Idadi ya makala:106,412
Idadi ya kurasa zote:212,419 (pamoja na kurasa za watumiaji, majadiliano, msaada n.k.)
Katikamwezi wa Agosti 2025 wikipedia ya Kiswahili iliangaliwa mara milioni 7.79 hivi, ambayo ni sawa na mara 251,607 kwa siku au mara 10,483 kila saa ambalo ni ongezeko la mara 4.5 ukilinganisha na mwaka 2024 mwezi wa Agosti. Asilimia 52 za wasomaji wetu wako Tanzania, asilimia 13 wako Kenya, asilimia 18 wako Marekani na mnamo asilimia 10 wako Ulaya.
(fungua anwani kwa browser yako, ondoa majina yaliyopo na ingiza jina la makala (hadi makala 10) unayopenda. Unaweza kubadilisha kipindi cha taarifa utakachoona; takwimu kabla ya 2015hapa)
na makala 100 zilizotazamiwa zaidi"Topviews" kwa kipindi fulani.
(unachagua kati ya makala 100 kwa mwezi au kwa siku)
Kamusi elezo ya Wiki ni kamusi elezo huru iliyo chini yaShirika Lisilo la Kiserikali laWikimedia Foundation, ambalo linasimamia miradi mingine mbalimbali ambayo imeorodheshwa hapo chini. Mpaka sasa miradi inayopatikana Kiswahili ni Wikipedia na Wikamusi. Wikitabu imewekwa Kiswahili lakini bado ni tupu. Mengine inapatikana Kiingereza pamoja na lugha tofauti.