Samia Suluhu Hassan (alizaliwa27 Januari1960) niRais wa 6 waTanzania na mwanachama wachama tawala chaChama Cha Mapinduzi. Kabla ya kuwa rais kutokana nakifo chaJohn Magufuli, kilichotokeatarehe17 Machi2021, Suluhu alikuwamakamu wa rais kwa sababu ya kuwa mgombea mwenza katikaUchaguzi Mkuu wa 2015.
Tarehe5 Novemba 2015 aliapishwa kamamakamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwamwanamke wa kwanza kufikiacheo hicho, akarudia baada yauchaguzi mkuu wa tarehe29 Oktoba2020.
Sasa amekuwarais wa kwanzamwanamke na rais wa Pili kutokaZanzibar Wa kwanza Akiwa ni Ally Hassan Mwinyi Rais wa awamu ya Pili.
Suluhu alizaliwa katika Usultani wa Zanzibar.
Alisoma shule za msingi zaChwaka (Unguja),Ziwani (Pemba) naMahonda (Unguja) katika miaka ya 1966 hadi 1972.
Aliendelea na masomo ya sekondari shule za Ngambo, Unguja (1973-1975) na Lumumba, Unguja (1976)[3].
Baada ya kumaliza masomo yake ya sekondari mnamo 1977, aliajiriwa na Wizara ya Mipango na Maendeleo kama karani. Alifuata kozi fupi kadhaa. Mnamo 1986, alihitimu kutoka Taasisi ya Usimamizi wa Maendeleo (Chuo Kikuu cha Mzumbe cha leo) na diploma ya hali ya juu katika utawala wa umma.
Baada ya kuhitimu, aliajiriwa kwenye mradi uliofadhiliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (World Food Programme). Kati ya miaka 1992 na 1994, alisoma kwenyeChuo Kikuu cha Manchester,Uingereza na kuhitimu stashahada ya uzamili katika uchumi.
Mnamo mwaka 2015, alipata MSc yake katika Maendeleo ya Uchumi wa Jamii kupitia mpango wa pamoja kati ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania naChuo Kikuu cha Kusini mwa New Hampshire.►Soma zaidi