Mama na mtoto wakifurahi pamoja.Monumento a la Madre (yaaniMnara kwa heshima ya Mama) hukoMexico City. Maandishi yake yanasema: "Kwa yule aliyetupenda kabla hajakutana nasi".Upendo ulivyochorwa naMfaransaWilliam-Adolphe Bouguereau.
Mama nimwanamke anayemleamtoto hasaaliyemzaa mwenyewe, lakini pengine sivyo, lakini anamlea. Upande wa pili anatarajiwa kuwepobaba, yaanimwanamume aliyeshirikiana naye katika kuzaa au anashirikiana naye katika kulea.
Wale ambao si wazazi wanaitwa ka kawaida "mama wa kambo" na "baba wa kambo".
Katikahistoria nautamaduni wa makabila na mataifa mengi, umama ni sifa maalumu ya mwanamke inayotangaza kuwa amekomaa na kukamilika kwa kuendelezauhai wabinadamu kadiri anavyoelekezwa naumbile lake upande wamwili na wanafsi.
Wastani waidadi ya watoto wanaozaliwa na mwanamke mmoja unatofautiana sana:mwaka2013 ule mkubwa zaidi ulipatikanaNiger (7.03 watoto waliozaliwa na kila mwanamke) na ule ndogo zaidiSingapore (0.79 tu).[1]
Jina hilo au lingine la kufanana linatumika katikalugha nyingi duniani, kwa sababu "neno la kwanza" la mtoto ni "ma" au "mama".
Kwa Kiswahili neno "mama" pia hutumika kama neno la heshima kwa wanawake hasa wa umri mkubwa kiasi. Mara nyingi hutumiwa pia ndani ya familia na mume kumwita mke wake.